Agosti 12: Historia na Mandhari ya Siku ya Kimataifa ya Vijana mwaka huu

Sherehe za siku hii zinakuja wakati ambapo Gen Z katika mataifa kama Kenya, Uganda, Bangladesh wamesimama kidete katika maandamano ya kupinga utawala mbaya katika serikali za nchi zao.

Muhtasari

• Iliadhimishwa kwa mara ya kwanza mnamo Agosti 12, 2000, na tangu wakati huo, siku hiyo imekuwa ikitumiwa kuelimisha umma kwa ujumla.

• Mnamo 1965, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilianza kufanya kazi kwa bidii ili kuelimisha na kuhamasisha vijana

SIKU YA KIMATAIFA YA VIJANA
SIKU YA KIMATAIFA YA VIJANA
Image: UN

Siku ya Kimataifa ya Vijana huadhimishwa Agosti 12 kila mwaka.

Inaadhimishwa kuashiria michango ya vijana katika maendeleo ya jamii sambamba na kuelewa changamoto zinazowakabili.

Siku hii huadhimishwa kupitia kampeni mbalimbali za uhamasishaji, matamasha ya jamii, na matukio ili kujulisha masuala ya kijamii, kiuchumi na kijamii na kisiasa ambayo vijana katika kila taifa wanakabiliana nayo.

Umoja wa Mataifa ulitangaza mwaka 1999 kuwa Agosti 12 itakuwa ni Siku ya Kimataifa ya Vijana.

Ilitokana na pendekezo kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lililotolewa na Mkutano wa Ulimwengu wa Mawaziri Wanaowajibika kwa Vijana huko Lisbon mnamo Desemba 17, 1999.

Iliadhimishwa kwa mara ya kwanza mnamo Agosti 12, 2000, na tangu wakati huo, siku hiyo imekuwa ikitumiwa kuelimisha umma kwa ujumla.

Mnamo 1965, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilianza kufanya kazi kwa bidii ili kuelimisha na kuhamasisha vijana.

Waliidhinisha tamko la kukuza maadili ya amani, heshima kwa wengine, na uelewa wa kitamaduni.

Kila mwaka, Siku ya Kimataifa ya Vijana huzingatia mada maalum ambayo huangazia nyanja tofauti za kuwawezesha na kuwalea vijana.

Mnamo 2024, mada iliyochaguliwa ni 'Kutoka kwa Mibofyo hadi Maendeleo: Njia za Kidijitali za Vijana kwa Maendeleo Endelevu'.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, mada hiyo ilijadili uhusiano kati ya "uwekaji digitali na kuharakisha maendeleo ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), ikisisitiza michango muhimu ya vijana katika mchakato huu wa mabadiliko."

Nchini Kenya, vijana wa kizazi cha Gen Z Jumapili waliandaa tamasha la kusherehekea siku ya kimataifa ya vijana jijini Nairobi kwa jina ‘Gen Sisi’ lililofanyika katika kituo cha magari cha Greenpark Terminus.

Tamasha hilo lilihudhuriwa na wasanii mbalimbali akiwemo Juliani, Khaligraph Jones, Mercy Masika, Nadia Mukami, Arrow Bwoy miongoni mwa wengine.

Sherehe za siku hii zinakuja wakati ambapo Gen Z katika mataifa kama Kenya, Uganda, Bangladesh wamesimama kidete katika maandamano ya kupinga utawala mbaya katika serikali za nchi zao.