Terence Creative kusimamia 'honeymoon' ya Sherman na Kendi

'honeymoon ni mimi nasimamia....nitawasimamia na Bonfire."

Muhtasari

•Mbunifu wa maudhui Terence Creative amesema atasaidia safari ya mwanzo ya harusi (honeymoon) ya Tony Sherman na Kendi.

•Tony na Kendi walipatana wakati wa maandamano ya kupinga serikali na wakapendana.

•Wawili hao wamepanga kufanya harusi tarehe 25, Agosti katika jiji la Nairobi.

Sherman Tony, Kendi the maandamano couple
Sherman Tony, Kendi the maandamano couple
Image: Sherman Tony, Kendi//Facebook

Mbunifu wa maudhui Terence Creative amesema ameahidi kusaidia safari ya mwanzo ya harusi (honeymoon) ya Tony Sherman na Kendi. Wawili hao walikutana wakati wa maandamano ya kupinga serikali na wameamua kuoana Junapili, Agosti 25.

Terence atasaidia kushirikiana na Bonfire Adventures ili kutuma wanandoa hao Mombasa baada ya harusi.

Wanandoa hao walipata umakini baada ya kufichua hadithi yao ya upendo ya kipekee.Walikutana wakati wa maandamano ya kupinga serikali jijini Nairobi na mara moja wakapendana.

Baada ya miezi mitatu, Sherman alipendekeza na sasa wamepanga kuoana. Shermanna Kendi wamekusudia kuoana Jumapili Agosti 25, katika sherehe ya umma kwenye eneo hilo ambapo walikutana mara ya kwanza.

Kwa video iliyoshirikishwa na Sherman Tiktok, Terence Creative alieleza msaada wake kwa wanandoa hao na kutangaza ya kwamba ataongea na Bonfire Adventures ili kusaidia safari ya mwanzo ya harusi.

Kwenye video Terence amesikika akisema "Honeymoon tutakuweka pale Mombasa.....Congratulation Sherman Tony, na salimia mama sana...kwa hivyo honemoon ni kwangu......Nitasimamia hiyo.......honeymoon ni mimi nasimamia....nitawasimamia na Bonfire."