Morara Kebaso: Ruto amenipa ofa ya kazi serikalini lakini nimekataa!

Wakili huyo amekuwa maarufu katika wiki za hivi karibuni kufuatia ziara zake katika maeneo mbalimbali kote nchini akitumbua miradi ambayo ilizinduliwa siku nyingi tu zilizopita lakini haikukamilika

Muhtasari

• “Sitaki kusema uwongo. Nimepokea ofa za kujiunga na serikali hata kutoka kwa rais mwenyewe," alisema.

MORARA KEBASO
MORARA KEBASO
Image: x

Morara Kebaso, jamaa anayetembea kote nchini kutumbua miradi hewa ya serikali sasa anadai amepokea ofa mbalimbali za kazi kutoka upande wa serikali, akiwemo rais Ruto.

Kupitia ukurasa wa X, Kebaso alichapisha ujumbe huo akifichua kwamba hata rais Ruto mwenyewe amempa ofa ya kujiunga na serikali, jambo ambalo hata hivyo alisema kwamba alikataa na kumuambia kuwa yuko sawa.

“Sitaki kusema uwongo. Nimepokea ofa za kujiunga na serikali hata kutoka kwa rais mwenyewe lakini nikamwambia niko sawa tu,” Kebaso alisema.

Wakili huyo amekuwa maarufu katika wiki za hivi karibuni kufuatia ziara zake katika maeneo mbalimbali kote nchini akitumbua miradi ambayo ilizinduliwa siku nyingi tu zilizopita lakini haikukamilika.

Miradi hewa ambayo Kebaso amekuwa akitumbua ni ile ya uzinduzi wa barabara ambazo zimesalia kuwa kama zilivyokuwa miezi kadhaa baada ya rais kuzizindua na kuweka jiwe la msingi.

Amekuwa katika mstari wa mbele kushtumu uongozi wa Kenya Kwanza kwa kile anadai ni uzinduzi wa miradi hewa ambayo inasalia kuzinduliwa kwa karatasi tu na picha lakini kwa uhalisia, hakuna kazi inayofanyika katika miradi hiyo.