Meru: Kanisa lachomwa pasta akituhumiwa kunyonya maziwa ya waumini wakati wa ibada

"Wakati mwingine angeweza kunyonya maziwa ya wanawake na watoto na kunyoa nywele zao sehemu za siri na kuweka nywele akidai atazitumia kuwaombea" mmoja alidai.

Muhtasari

• Aidha walidai kuwa alikuwa ameajiri baadhi ya wahudumu ambao wangemsaidia kunyonya maziwa ya watoto wadogo

Picha ya nyumba inayowaka moto
Image: Hisani

Wanakijiji wenye gaghabu walivamia kanisa moja huko kaunti ya Meru na kuliteketeza kanisa moja kwa kile walidai kwamba mchungaji wa kanisa hilo amekuwea na hulka ya kuwanyanyasa waumini wa kike.

Kwa mujibu wa runinga ya K24, wanakijiji walimshtumu mhubiri huyo kwa kile walisema ni mazoea yake ya kunyonya maziwa ya waumini wakati wa ibada.

Wanakijiji hao waliambia runinga hiyo kwamba mhubiri huyo amekuwa akitekeleza unyanyasaji huo kwa miaka 10 sasa.

Mwanamke mmoja, muumini wa zamani wa kanisa hilo, alisema mshukiwa kuwa mwanamume mwenye utata wa kitambaa hicho amekuwa akiwalazimisha waumini kufanya mambo ya ajabu kwa jina la kuwaombea.

"Nilikuwa mmoja wa washiriki wa kanisa lake lakini wakati fulani niligundua alikuwa akifanya uchawi badala ya kuhubiri neno la Mungu nilipoondoka mwaka jana," alinukuliwa na kituo hicho cha runinga.

Baada ya kuchoma moto kanisa lake siku ya Jumanne, wanakijiji hao na waumini wa kanisa hilo pia walimtuhumu mchungaji huyo kwa kuwanyoa wafuasi wake nywele za sehemu ya siri huku akiimba maneno yasiyo ya kawaida.

"Mambo ya ajabu yamekuwa yakitokea katika kanisa hili lakini hatuwezi kujua kwa nini tuliendelea kwenda kanisani licha ya matukio haya yote ya kutisha, wakati mwingine anaweza kuchinja mbuzi au kuku na kupaka damu kwenye miili ya watu huku akizungumza maneno ya kuchekesha; wakati mwingine angeweza kunyonya maziwa ya wanawake na watoto na kunyoa nywele zao sehemu za siri na kuweka nywele akidai atazitumia kuwaombea. Nadhani ni mchawi, si mchungaji,” mmoja wa waumini wa kanisa hilo aliongeza.

Aidha walidai kuwa alikuwa ameajiri baadhi ya wahudumu ambao wangemsaidia kunyonya maziwa ya watoto wadogo.

Akizungumza baada ya kurekodi taarifa katika afisi za DCI mwinjilisti huyo mwenye utata aliambia K24 kwamba shutuma hizo si za kweli na kuwataka polisi kufanya uchunguzi.

"Nimekuwa nikihubiri kwa miaka 20 iliyopita na yote wanayosema sio kweli sheria inapaswa kuchukua mkondo wake kwa sababu wamechoma kanisa na kuharibu mali ya Ksh5 milioni," Mururu alisema.