Mume akiri kumwekea mkewe sumu kwenye soda akilenga kumuua ili kuoa binti yake

Mzee huyo wa miaka 71 alikiri kwamba sumu hiyo alikuwa anajaribu kumuua nayo mkewe wa miaka 51 alikuwa amepewa na binti yake wa miaka 31 ambaye alilenga kumuoa baada ya mamake kufa.

Muhtasari

• Kabla ya kuwasiliana na polisi, Bishop alilazwa hospitalini mara sita katika kipindi cha wiki chache.

• Alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya kichwa yasiyoelezeka, kusinzia, kuhara, na dalili nyingine za ajabu.

Image: BBC News

Mwanamume wa Indiana amekiri kuweka sumu kwenye kinywaji aina ya soda katika kikombe ambacho mkewe alikusudia kutumia akilenga kumuua.

Kwa mujibu wa Daily Mail, mzee huyo kwa jina Alfred Ruf mwenye umri wa miaka 71 alihukumiwa kifungo cha miaka minne jela baada ya kukiri kosa la kutaka kusababisha hatari ya kifo. 

Mashtaka dhidi ya mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 71 yalitokana na msururu wa matukio ya mwaka wa 2021, ambapo aliripotiwa kumwagia sumu vinywaji baridi vya mkewe mara kumi na mbili.

Kufikia Januari 2022, Ruf alikuwa anachunguzwa baada ya mkewe, Liza Bishop, 51, kufahamisha mamlaka kwamba alidhani mumewe alikuwa akijaribu kumtilia sumu.

Kabla ya kuwasiliana na polisi, Bishop alilazwa hospitalini mara sita katika kipindi cha wiki chache.

Alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya kichwa yasiyoelezeka, kusinzia, kuhara, na dalili nyingine za ajabu.

Wakati wa kila kukaa hospitalini, alipimwa na kukutwa na dawa kama vile cocaine, MDMA, na benzodiazepines, ambayo hakuna hata moja ambayo alikuwa ametumika awali.

Wakati fulani, Bishoppia aligundua mabaki ya unga kwenye chupa zake za soda.

Ruf baadaye alikiri kwa mkewe kwamba kweli alikuwa akijaribu kumtia sumu kwa sababu 'alihisi vibaya' kuhusu hilo. Baadaye, aliwasiliana na watekelezaji wa sheria.

Wakati mamlaka ilipojibu nyumbani kwa wanandoa hao, inasemekana walimsikia Ruf akitaja kuwa alikuwa 'akinywesha' kinywaji cha mkewe na 'kitu kisichojulikana' alichopokea kutoka kwa binti yake wa miaka 31.

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 71 alipelekwa katika idara ya Sherifu wa Kaunti ya Wayne, ambapo inaonekana alikiri kuhusika na mauaji hayo wakati wa mahojiano.

Pia inasemekana alikiri kuwa na uhusiano wa kimapenzi na binti wa Bishop kutoka kwa ndoa ya awali.