Drama baada ya jamaa kukutana na mkewe 'marehemu' akiwa na mwanaume mwingine

Mpenzi mpya wa mwanamke huyo anadaiwa kuzirai mara mbili baada ya kushuhudia tukio hilo.

Muhtasari

•Tamuno Douglas anadaiwa kumuona 'marehemu' mkewe mjini Yenagoa ambako alikuwa amelikwa kwa mahojiano ya kazi.

•Douglas alidai kuwa mke huyo wake aliaga na kuzikwa baada ya kupambana na ugonjwa wa Asthma kwa muda.

Image: HISANI

Mwanaume mmoja kutoka Nigeria anaripotiwa kusababisha drama kubwa barabarani baada ya kukutana na mkewe ambaye alifariki miaka mitatu iliyopita akiwa ameshikana na mwanaume mwingine.

Katika kisa kilichosimuliwa  kwenye Twitter, jamaa aliyetambulishwa kama  Tamuno Douglas anadaiwa kumuona 'marehemu' mkewe mjini Yenagoa ambako alikuwa amelikwa kwa mahojiano ya kazi.

"Bw Douglas alisema alikuja Yenagoa jana kwa Mahojiano katika Hospitali iliyo karibu na akaamua kuzunguka ili kuona jinsi Yenagoa inafanana. Alikuwa akizungukazungukkwenye mzunguko wa Opolo alipomwona mkewe aliyefariki miaka 3 iliyopita katika mji wake wa nyumbani," @Ebiowei_C alisimulia.

Jamaa huyo alimuona mkewe na mwanaume anayeaminika kuwa mpenziwe wakiabiri Tuktuk, tukio ambalo lilimshangaza sana.

Alidai kuwa mke huyo wake aliaga na kuzikwa baada ya kupambana na ugonjwa wa Asthma kwa muda.

"Mara ya kwanza nilisita, kisha nilipata ujasiri na kumwita kwa jina, akageuka, akanitazama na kutoweka," Bw Douglas alisema alipohojiwa.

Mpenzi mpya wa mwanamke huyo anadaiwa kuzirai  mara mbili baada ya kushuhudia tukio hilo la kushangaza.

Alisema amekuwa akiishi na mwanamke huyo kwa zaidi ya mwaka mmoja baada ya kukutana kanisani na baadae kumvisha pete ya uchumba.

Tukio hilo linasemekana kuvuta umati mkubwa  na kusababisha msongamano wa magari katika Barabara ya Opolo-Elebele huko Yenagoa.

Kwa miaka mingi visa vingi vya kustaajabisha na vingine vya kuogofya vimeripotiwa katika nchi ya Nigeria.

Nchi hiyo ya Afrika Magharibi hudaiwa kuwa na visa vingi vya uchawi na ibada za miungu tofauti. Filamu zao nyingi zinazohusisha shughuli kama hizo pia zimefanya dhana kuaminika na wengi.