Mwanaume amfumania mkewe mjamzito akishiriki tendo la ndoa hospitalini na mwanaume mwingine

Mwanamke huyo mjamzito alikuwa amelazwa hospitalini kwa wiki moja akisema anaumwa Malaria.

Muhtasari

• Mwanaume huyo aliyefumaniwa na mke wa mtu alisemekana kuwa muuza nyama na mishikaki.

• Polisi waliwahi na kumchukua mtuhumiwa ambaye walisema atashtakiwa kwa kuzua kero kwa umma.

Image: GETTY IMAGES

Mwanamume mmoja nchini Uganda alimfumania mke wake mjamzito akishiriki kitendo cha mapenzi na mwanaume mwingine katika kitanda cha hospitali moja nchini humo.

Kulingana na taarifa zilizochapishwa na majarida mbalimbali, mwanamke huyo mjamzito alikuwa ameenda hospitalini na alikuwa amelazwa kwa takribani wiki moja akisema alikuwa anaumwa Malalria.

Baadae ndio mume wake alimtembelea ‘mgonjwa’ wake na alichokiona kilimtoa pima machoni.

Alimfumania mkewe mjamzito akishiriki mapenzi na mwanaume mwingine kijana wa miaka 24.

“Nilifanya ziara ya kushtukiza hospitalini kumjulia hali mke wangu ndipo nikamkuta mwanaume huyo kitandani na mke wangu mjamzito. Alikuwa amelazwa kwa sababu alikuwa anaugua malaria,” Alex aliambia The Monitor.

Polisi walipofika hospitalini hapo awali hawakujua ni mashtaka gani wangemfungulia mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 24, muuza nyama choma anayefanya kazi katika mji wa Apac, kabla ya kumalizana na shtaka la kusababisha kero kwa umma.

"Tumependelea mashtaka ya kusababisha kero ya umma dhidi ya mshukiwa, lakini bado tunachunguza na tutawapa taarifa kwa wakati ufaao," David Wills Ndaula, kamanda wa polisi wa Wilaya ya Apac, alisema kuhusu tukio hilo lililotokea wiki iliyopita.

Mwanamume huyo kwa sasa anashikiliwa na polisi huku uchunguzi ukiendelea.

 Tukio hili linajili wiki kadhaa baada ya tukio kama hilo kuripotiwa nchini Zambia ambapo mwanaume alimfumani mkewe mjamzito akishiriki mapenzi na mwanaume mwingine ndani ya chumba chao cha malazi.

Mwanaume huyo ambaye alirekodi video hiyo ambayo ilisambaa alisema kuwa alikuwa ameaga mkewe kuwa anaondoka safarini lakini akafika njiani na kuahirisha safari.

Aliporudi nyumbani alimkuta mwanaume mchungaji ambaye pia anafanya uganga wa kienyeji akiwa kitandani mwake na mke wake – wote wakiwa uchi wa hayawani.