Viongozi wa kidini wanataka kusitishwa kwa uhasama

Juhudi zaimarishwa kumaliza uhasama kati ya Uhuru na Ruto

Jamii ya kimataifa inahofishwa na kupanda kwa joto la kisiasa

Muhtasari

 

  • Tofauti kati ta Uhuru na Ruto zimetokana na siasa za urithi wa 2022
  •  Ruto ameonekana kutengwa na masuala ya serikali na hivyo basi kuamua kujitosa katika kampeini 
  •  Rais amehamakishwa na matusi ya washirika wa DP dhidi yake na familia yake 

 

Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto

Jitihada mpya na za dharura zimeanza kufanywa ili kumaliza tofauti kati ya rais Uhuru kenyatta na naibu wake William Ruto huku jamii ya kimataifa ikizua hofu kuhusu  kupanda kwa joto la kisiasa .

 Maelezo kuhusu juhudi hizo za kuwapatanisha yametolewa siku chache baada ya hafla ya maombi ya kitaifa siku ya  Jumamosi ambapo tofauti kati ya viongozi hao zilidhihirika.

 Itifiki ilipuuzwa huku kila mmoja akiondoka kupitia njia tofauti.  Septemba tarehe 28 Ruto alikosa kuhudhuria  kongamano la kitaifa la Covid 19  ishara kwamba uhusiano wake na mkuu wake umezorota sana.

 
 

 Duru zaarifu kwamba kundi moja la viongozi wa kidini wenye ushawishi mkubwa limekutana na rais  na naibu wake  kando kando na  wawili hao walitarajiwa kuandaa kikao na wanahabari ili kutangaza kusitisha uhasama na ‘bifu’ iliyopo kati ya kambi zao za kisiasa .

 Viongozi hao wa kidini walikutana na rais Kenyatta Alhamisi wiki iliyopita. Rais inadaiwa alihamakishwa na matusi ambayo washirika wa Ruto wanamwelekezea pamoja na familia yake miongoni mwa masuala mengine .

 Wiki jana binamu yake rais Uhuru Beth Mugo alimhusisha Ruto na mashambulizi hayo akisema naibu wa rais hakujitokeza wazi kulaani vitendo vya washirika wake wa kisiasa.

 “…Kwa sababu nahodha wao wa kisiasa naibu wa rais hajajitokeza kulaani matusi ya washirika wake  dhidi ya rais Kenyatta, ni  ishara tosha. Je, yamaanisha kwamba DP anaunga mkono matamshi ya viongozi hawa?’ Mugo aliuliza.

 Siku ya Jumatatu kundi la viongozi wa kidini lilifanya mkutano uliodumu saa tano na naibu wa rais Ruto  katika makazi yake rasmi ya Karen.

Duru katika afisi ya Ruto zasema kundi hilo liliongozwa na  Askofu mkuu wa Nyeri Anthony Muheria  na kuwahusisha  wengine kama  askofu mstaafu wa AIC Silas Yego  na askofu wa CITAM David Oginde.

 Kwa sababu ya mkutano huo Ruto alilazimika kusafiri kwa ndege kutoka nyumbani kwake Sugoi huko Uasin Gishu ili kurejea jijini baada ya kuwaalika nyumbani kwake viongoz kutoka Nyanza siku hiyo.

 
 

(Mhariri Davis Ojiambo)