Matiang'i apondwa Kisii na Nyamira

Matiang’i apondwa na washirika wa Ruto katika ziara ya Nyamira

DP Ruto alikosa kufanya ziara yake katika maeneo hayo wiki jana

Muhtasari
  •  Viongozi hao wamesema hawatotishwa na serikali kuhusu kumuunga mkono Ruto 
  •  Waapa kuendelea na mikutano ya kuwasaidia mahasla 
  •  Wamshtumu Matiang'i kwa kutoisadia jamii  ya Wakisii licha ya kuwa madarakani 

 

Washirika wa kisiasa wa naibu wa rais William Ruto wameishtumu serikali kwa  kuwatishgia viongozi ambao wanamuunga mkono naibu wa rais William Ruto na kundi lake la  ‘Hustler’

 Wakizungumza katika hafla iliyohudhuriwa na Ruto huko Nyamira ,mbunge wa Mathira  Rigathi Gachagua  alimshtumu waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang’I  kwa kuwatumia polisi kuwatupia vitoa machozi wafuasi wa Ruto  wiki jana akidai kwamba Matiang’i hajaisadia jamii hiyo .

" Ni watu wangapi  ambao mtu weni amewasaidia kupata kazi katika serikali  ,KWS , magereza na hata  uhamasishaji  ilhali najiita kiongozi .Maamlaka ni ya muda  yatumie kuwasaidia maskini’ amesema siku ya  alhamisi

 Washirika wa Ruto sasa wanaitaka serikali kuziomba msamaha familia mabazo ziliwapoteza jamaa zao katika machafuko ya Murang’a wiki jana na kuzifidia .

Ruto ameandamana na naibu gavana wa KISII  Joash Maangi ,   Mbunge wa  Kitutu Masaba Shadrack Mose, Vincent Kemosi waWest Mugirango, Joash Nyamoko (North Mugirango), na Silvanus Osoro (South Mugirango).

 Wengine  ni seneta mteule  Milicent Omanga, mbunge wa Kiharu  Dindi Nyoro, Rigathi Gachagua (Mathira)  na mfanyibiashara  Don Bosco pamoja na wakilishi wa kauti kutoka Nyamira na Kisii .

 Viongozi hao wamesema wanamuunga mkono naiu wa rais William Ruto  na vitisho vya serikali havitawatikisa katika msimamo wao huo .

" Kama wabunge na wanachaa wa  vugu vugu la hustler ,tupigana  kwa kila njia kuhakikisha kwamba unakuwa rais’ amsema mbunge Mose

 Mbunge wa North Mugirango Joash Nyamoko  amesema naibu wa rais ataendelea kuwasaidia watu ambao ni mahasla nchini

Nyoro amesema washirika wa DP waliondolewa kutoka kamati za bunge kwa sababu ya msimamo wao wa kumuunga mkono .

Alimthubutu waziri wa usalama wa ndani Fred mtaiang’I kumkamata kwa sababu alikuwa katika eneo la Gusii .