Ruto Ziarani Kisii na Nyamira

Wanaojaribu kuzuia mkutano wangu Kisii ni ‘wajinga’-Ruto

Anafanya ziara hiyo baada ya polisi kuwazuia wafuasi wake katika maeneo ya ikutano wiki jana

Muhtasari

 

  •  Ruto awalaumu baadhi ya watu serikali kwa kuzuia mikutano yake 
  • Asema  hana tatizo na polisi wkani wanafanya kazi kuzilisha familia zao 
  •  Asema hatokoma kuendelea kuwasaidia watu wa kawaida 

 

DP William Ruto

 

 Naibu wa rais William Ruto amesema  maafisa wa polisi ni watu wazuri ambao wanazitafutia familia zao a. Akizungumza huko Nyamira  siku ya alhamisi Ruto  amesema mkutano wake huo uliofaa kufanyika wiki jana ulizuiwa na baadhi ya viongozi ambao hawajapendezwa na vugu vugu lake la Hasla .

" Hawa pollisi hawana shida . Shida  ni watu wanaoishi katika minara  mirefu bila kujua shida za watu wengine’ Ruto amesema

 

 Ruto amesema  hatozuiwa kuendeea na dhamira yake kusaidia watu  wanaofanya kazi katika sekta ya boda boda na biashara nyingine ndogo ndogo .

" Wale wanajaribu kuzuia ziara yangu ya Kisii ni wajinga .watu kama hao ni wakabila . Kila mkenya naruhsiwa kuzuru sehemu yoyote nchin’

 Amewarai viongozi kuepuka siasa za kikabila .

" Acheni kuwagawanya wakenya .hakuna mkenya ambaye ni mgeni katika sehemu yoyote ya nchi’

 Ruto amesema  siasa zinafaa kuwaangazi watu wa kawiada kabla ya kujadili masuala ya siasa za watu kujipa viti na maamlaka .

Amesema serikali ya Jubilee iliundwa ili kuwaunganisha wakenya wote ikiwemo kuwapa nafasi za kazi kwa watu wa Kisii na Nyamira .

 Ruto ameandamana na naibu gavana wa KISII  Joash Maangi ,   Mbunge wa  Kitutu Masaba Shadrack Mose, Vincent Kemosi waWest Mugirango, Joash Nyamoko (North Mugirango), na Silvanus Osoro (South Mugirango).

 

 Wengine  ni seneta mteule  Milicent Omanga, mbunge wa Kiharu  Dindi Nyoro, Rigathi Gachagua (Mathira)  na mfanyibiashara  Don Bosco pamoja na wakilishi wa kauti kutoka Nyamira na Kisii . Viongozi hao wameapa kumuunga mkono Ruto katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022