Dj Evolve aomba kuondoa kesi yake mahakamani

Muhtasari
  • DJ Evolve alipigwa risasi na mbunge wa Embakasi Babu Owino
  • Evolve anaomba kuondoa kesi yake dhidi ya mbunge huyo

Mcheza deki Felix Orinda almaarufu DJ Evolve ameomba kuondoa kesi yake mahakamani, hii ni baada ya mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino kumpiga risasi mapema mwaka huu.

Evolve alisema kuwa ameamua hayo baada ya kushauriana na familia yake, alisema kuwa familia yake iliamua kuzingatia afya yake na wala si kesi ambayo imo mahakamani.

Kupitia barua yake Evolve kwa mahakama ilisoma kuwa kesi hiyo imeathiri uponyaji wake.

 

Hata hivyo mkurugenzi wa mashtaka ya umma DPP alisema kuwa anataka muda zaidi ili kuchunguza akili ya Evolve ili aweze kujibu barua hiyo.

korti ilisema kuwa Evolve aliwasiliana nao bali hakusikika vyema kwa maana alikuwa na tubu ambayo alikuwa amewekwa mdomoni mwake.

Pia barua hiyo ilikuwa na kichapo cha kidole cha gumba ili kuthibitisha mwathiriwa huyo alitia saini.

Kwa uamuzi wake Mchoi alisema kuwa aliona barua ya Evolve akisihi kuondoa kesi dhidi ya mbunge Babu Owino.