Covid-19: Watu 12 waaga dunia huku 616 wakipatikana na corona

Muhtasari
  • Watu 104 wapona corona huku 12 wakipoteza maisha yao kutokana na virusi hivyo
  • 616 wamepatikana na virusi vya corona
kagwe
kagwe

Watu 12 hii leo wamepoteza maisha yao kutokana na virusi vya corona na kufikisha idadi jumla ya 825 walioaga dunia kutokana na corona.

Huku hayo yakijiri watu 616 wamepatikana na virusi hivyo na kufikisha idadi jumla ya  44,196 watu walioambukizwa corona hii ni baada ya sampuli 5,512 kupimwa kati ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo mapya 594 ni wakenya huku 22 wakiwa raia wa kigeni,391 ni wanaume ilhali 225 ni wanawake.

Mgonjwa mwenye umri wa chini ana miezi nane huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 86 amesema waziri wa afya Mutahi Kagwe.

Vile vile watu 104 wamepona virusi hivyo na kufikisha idadi jumla ya 31,752 ya watu waliopona corona.