Covid-19: Watu 227 wapona corona huku 7 Wakipoteza maisha yao

Muhtasari
  • Watu 195 wapatikana na corona huku idadi ya maambukizi ikifika 45,076
  • 7 wamefariki kutokana na corona
  • 227 wapona Covid-19 chini ya saa 24 zilizopita 
IMG-20200318-WA0008 (3) (1)
IMG-20200318-WA0008 (3) (1)

Watu 227 wamepona virusi vya corona na kufikisha idadi ya jumla ya  watu 32,084 waliopona virusi vya corona, 146 waliopona walikuwa wakipokea matibabu nyumbani ilhali 81 walikuwa hospitalini.

Huku hayo yakijiri watu 7 wamepoteza maisha yao na kufikisha 839 idadi ya watu waliofariki  kutoka na virusi vya corona nchini Kenya.

Wakati huo huo watu 195 wamepatikana na corona hii leo Jumatatu na kufikisha idadi ya jumla ya watu 45,076 walioambukizwa corona. 

 

Kati ya maambukizi hayo mapya 137 ni wanaume huku 58 wakiwa ni wanawake, mgonjwa wa umri wa chini ana miezi mitano huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 75.

Watu 39 wako katika hali mbaya na wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi huku wengine 39 wakitumia oksijeni amesema waziri wa afya Mutahi Kagwe.

(Mhariri Davis Ojiambo)