Makao makuu ya kaunti ya Nandi yafungwa baada ya wafanyakazi 8 kupatikana na corona

Muhtasari
  • Makao makuu ya kaunti ya Nandi kufungwa kwa muda wa siku 14
  • Wafanyakazi,8 wapatikana na virusi vya corona

Makao makuu ya kaunti ya Nandi yamefungwa kwa muda wa wiki mbili hii ni baada ya wafanyakazi wa makao hayo kupatikana na virusi vya corona.

Serikali ya kaunti hiyo iliwashauri wafanyakazi kufanyia kazi nyumbani kuanzia jumatatu 19 Oktoba ii kuthibiti kuenea kwa virusi hivyo.

Kulingana na barua ilioandikwa na serikali ya kaunti hiyo sita walioambukizwa virusi hivyo ni wa kutoka katika idara ya kifedha na mipango ya kiuchumi.

 

Katibu Mkuu wa kaunti hiyo Francis Sang alisema kwamba wafanyakazi wale wengine wote watapimwa virusi vya corona huku afisi za kaunti hiyo zikinyunyiziwa dawa.

"Wafanyakazi wa Idara zilizotajwa watafanyia kazi nyumbanikwa muda wa siku kumi na nne kuanzia Jumatatu 19." Baadhi ya taarifa ilisoma.