Covid 19

16 wafariki huku 497 wakipatikana na corona

Watu 858 wameaga dunia hadi sasa

Muhtasari
  • Nairobi inaongoza kwa visa 227 
  • Idadi ya walioaga dunia leo ni 16 

 

Mutahi Kagwe
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe Mutahi Kagwe

Watu 497 wamepatikana na virusi vya corona  baada ya sampuli 4,888 kupimwa katika saa 24 zilizopita .Idadi hiyo sasa inafikisha 46,144 jumla ya visa vya ugonjwa huo nchini . Jumla ya sampuli zilizopimwa hadi sasa ni 632,669.Kutoka visa hivyo 471 ni vya wakenya huku 26 vikiwa vya raia wa kigeni .mgonjwa wa umri wa chini  ni mtoto wa mwaka mmoja ilhali wa umri wa juu ana  umri wa miaka 88 .

 Watu 295 waliopatikana na ugonjwa huo ni wanaume ilhali 202 ni wanawake

 Leo watu 238 wamepona  na kufikisha jumla ya watu waliopona corona nchini kuwa 32,760 .

Hata hivyo watu 16 wameaga dunia na kufikisha idadi ya walioangamia kwa ajili ya corona kuwa 858 .

Kwa sasa kuna wagonjwa 27 katika kitengo cha wagonjwa mahtuti  ilhali 27 wapo katika usaidizi wa kupumua  na 41 wanasaidiwa  na gesi ya kupumua .