- Askari wa jela akamatwa na kadi za simu
- Ulaghai wa kupitia simu na mtandao umezidi nchini
Maafisa wa DCI wamemkamata afisa mmoja wa maghereza Constable Charles Opollo Ndaga katika mtaa wa Sinapanga huko Bondo kwa usajili haramu wa kadi za simu
Walipokagua nyumba yake walizipata kadi 10,000 za simu ,simu kadhaa za rununu na kitabu cha hundi . Kadi mbili za simu za Equitel na vitambulisho vitatu vilipatikana pia .
Mshukiwa yupo katika kizuizi cha polisi akingoja kufikishwa kortini . Katika tukio jingine kama hilo ,mshukiwa mmoja alikamatwa siku ya jumapili huko Taita taveta kwa ujasusi wa mtandaoni . mshukiwa huyo Archibald Kalela Mwandawiro mwenye umri wa miaka 52 alikamatwa Wundanyi ambapo polisi walinasa kifaa kinachotumiwa kunasa mawasiliano ya mtandao
Wakati wa oparesheni hiyo vifaa 25 vya modem ,kadi 83 za simu za airtel ,kadi 76 za simu za safaricom ,tarakilishi bebe na simu ya rununu pamoja na vifaa n vilinaswa