- Uhuru amesema wakenya wanafaa kuisoma na kuinga mkono ripoti ya BBI
- Amesema ripoti hiyo itawaunganisha wakenya
Rais Uhuru Kenyatta amewataka wakaazi wa kisumu kuunga mkono ripoti ya BBI . Uhuru siku ya alhamisi amewataka wakaazi kuisoma na kuielewa ripoti hiyo na kutembea pamoja na wakenya wengine kwani ripoti hiyo itawaunganisha wakenya .
Uhuru alikuwa akizungumza katika uwanja wa Kisumu Showground wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa uwanja wa Michezo wa kimataifa wa Jomo Kenyatta katika uwanja wa Mamboleo
amesema uwanja huo wa maonyesho utabadilishwa kuwa uwanja mkubwa wa michezo huku viwanja vingine vya michezo nchini vikifanyiwa ukarabati .
amesema baada ya uwanja huo kutamatika utakuwa mwenyeji wa mchuano mkali kati ya Gor Mahia na Afc Leopards aprili mwaka ujao .
" Tulikatathmini kwamba uwanja wa Jomo Kenyatta haukutosha kuwa wa kimataifa na ndiposa baada ya mashauriano na gavana na wadau wengine tuliamua kuubadilisha uwanja huo wa maonyesho kuwa uwanja wa kimataifa ‘Uhuru amesema
Uhuru amesema yeye na Raila wataongoza kampeini za kuwataka wakenya kuunga mkono ripoti ya BBI .