Uhuru cheza Jerusalema

Uhuru, Raila wadensi wimbo wa ‘Jerusalema’ katika ziara ya Kisumu

Rais alikuwa ziarani Kisumu

Muhtasari

 

  •  Wimbo wenyewe umewavutia watu muilioni 180 katika Youtube

 

Rais  Uhuru Kenyatta  siku ya alhamisi liamua kunengua mauno akicheza wimbo maarufu wa Jerusalema  wakati wa ziara yake mjini Kisumu akiwa ameandamana na kiongozi wa ODM Raila Odinga .

Akiwa amevalia shati la rangi ya samawati  rais alionekana akipiga mauno kutumia mtindo wake kabla ya  Raila kujiunga naye jukwaani pia kucheza .

 Gavana wa Kisumu  Anyang' Nyongo'  na viongozi wengine pia waliingilia kudensi huku wananchi wakiwashangilia . Uhuru  alikuwa katika uwanja wa maonyesho wa Mmbo leo ambao sasa umebadilishwa kuwa uwanja  wa Michezo .

 Wimbo huo wa Master KG na  Nomcebo Zikode,   umetajwa kama wimbo unaosisimua zaidi baada ya watu wengi sana kuucheza katika nchi mbali mbali na  tayari umetazamwa mara milioni 180 katika Youtube .