Hakuna pesa

Waziri Yatani akataa kutoa pesa za kuwalipa wafanyikazi waliotumwa kuitumia NMS

Yatani aikausha NMS

Muhtasari

 

  •  Yatani asema hazina ya kitaifa haiwezi kutoa pesa moja kwa moja hadi kwa NMS
  • Fedha hizo zinafaa kuisaidia NMS  kuwalipa wafanyikazi wake zaidi ya  6000 

 

Maamlaka ya kusimamia jiji la Nairobi  imepata pigo baada ya waziri wa fedha  Ukur Yatani kudinda kutoa pesa za kuwalipa  wafanyikazi zaidi ya 6000 waliotumwa kuifanyia kazi .

 Waziri Yattani amesema hakuna sheria inayohalalisha kutolewa kwa fedha za kuwalipa wafanyikazi hao  akisema fedha hizo zinaweza tu kutolewa kupitia serikali ya kaunti ya Nairobi kupitia   hazina ya  mapato ya kaunti .

 Katika barua  ilioandikwa kwa mkuu wa NMS Mohammed Badi  waziri Yatani amesema kila kaunti inastahili kupewa fedha kupitia hazina ya mapato kwa kaunti na itakuwa ukiukaji wa sheria kwa NMS kupewa fedha moja kwa moja kutoka kwa hazina ya kitaifa .

 Kando na utata huo wa fedha waziri Yattani amesema anagojea maelekezo kutoka kwa mkuu wa sheria kuhusu hatua zinazofaa kuchukuliwa .