Muhtasari
- Kutoka visa hivyo 596 ni vya wakenya ilhali 35 ni raia wa kigeni
- Kwa sasa kuna wagonjwa 20 katika kitengo cha ICU ,59 Wanasaidia kwa hewa ya kuumua ilhali 16 wapo katika kitengo cha HDU
Watu 631 wamepatikana na virusi vya corona siku ya ijumaa baada ya sampuli 6,142 kupimwa katika saa 24 zilizopita na kufikisha visa hivyo nchini kuwa 47,843 huku jumla ya sampuli zilizpimwa ikiwa 646,367 .
Kutoka visa hivyo 596 ni vya wakenya ilhali 35 ni raia wa kigeni .watu 420 kati ya wagonjwa hao ni wanaume ilhali 211 ni wanawake.Mgonjwa wa umri wa chini ni mtoto wa mwaka mmoja ilhali wa umri wa juu ana miaka 91 .
Hata hivyo watu 14 wameaga dunia kwa ajili ya ugonjwa huo na kufikisha idadi ya walioangamizwa na corona kuwa 884 .Kwa sasa kuna wagonjwa 20 katika kitengo cha ICU ,59 Wanasaidia kwa hewa ya kuumua ilhali 16 wapo katika kitengo cha hdu .