- Jumwa ameshtakiwa kwa mauaji
- Ametakiwa kusalimisha paspoti yake kortini
Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa ameachiliwa kwa bondi ya shilingi milioni 3 au dhamana ya shilingi milioni nne pesa taslimu
Mlinzi wake Geoffrey Otieno aliachiliwa kwa bondi ya shilingi milioni moja au dhamana mdadala ya shilingi milioni 1.5 pesa taslimu .
Jaji Njoki Mwangi amewaagiza washtakiwa kuwasilisha paspoti zao kortini . Amesema wataruhusiwa tu kusafiri endapo watatoa sababu tosha za kuruhusiwa kusafiri .
Mwangi pia amewaonya dhidi ya kuwatishia mashahidi wa upande wa mashtaka .Jumwa na msaidizi wake watatakiwa kufika kortini kila wakati mahakama itakapowataka kufanya hivo .
Jumwa ameshtakiwa pamoja na Otieno ka kumuua Gumbao Jola mwanamme mwenye umri wa miaka 48 katika kijiji cha Ganda Oktoba mwaka wa 2019 . Naibu mkurugenzi wa mashtaka ya umma wa Mombasa Alloys Kemo alipinga kuachiliwa kwa wawili hao wa dhamana .
Kemo amesema Jumwa ni mtu mwenye ushawishi mkubwa na atavuruga mashahidi wa upande wa mashtaka ambao wanategemewa katika kesi hiyo dhidi yake .Pia alisema Otieno hana makaazi ya kudumu na hivyo basi itakuwa ni hatari kwa mahakama kumuachilia huru .