- Baadhi ya wazazi wanahofia kuwaruhusu wanao kwenda shule
- Shule zilitarajiwa kufunguliwa kikamilifu wiki ijayo
Wizara ya elimu imeweka katika darubuni uwezekano wa kuzifungua kabisa shule na taasisi za masomo
Wanafunzi wa Gredi ya nne 4, darasa la 8 na kidato cha 4 walikuwa tayari wamerejea shuleni wiki mbili zilizopita . Lakini huenda shule zikafungwa tena kwa sababu ya kuongezeka kwa visa vya virusi vya corona na wanafunzi wengine walitarajiwa kuripoti shuleni jumatatu wiki ijayo.
Madarasa hayo matatu yanasheheni wanafunzi takriban milioni 2.8
Arifa ya muungano wa shule za kimataifa ya tarehe 22 inaonyesha kwamba wizara ya elimu huenda inalenga kubadilisha tangazo la hapo awali kuwaruhusu wanafunzi wengine kwenda shuleni .
Wakati wa awamu ya kwanza ya kuzifungua shule waziri wa Elimu George Magoha alizitaja siku 14 za kwanza kama muhimu za kukadiria iwapo taasisi za elimu ziko tayari kupambana na janga la corona .
Walimu wakuu waliagizwa kutafuta mianya na njia za kuisuluhisha .Pia walitakiwa kutathmini mahitaji ya kielimu ya wanafunzi kabla ya kuanza kuwasomesha .
Lakini maelezo katika arifa hiyo ya shule za kimataifa inaonyesha kwamba serikali huenda inapunguz akasi kuhusu mpango wake wa kuzifungua shule kikamilifu .
“ Kwa sababu ya ongezeko la visa vya covid 19 wizara ya elimu imeamua kuahirisha kufunguliwa kwa shule’ imesesema sehemu ya arifa hiyo .
Ongezeko la visa vya covid 19 limeaicha wizaa ya elimu katika njia panda iwapo patahitajika tena kufungwa kwa shule .Duru zaarifu kwamba pana hofu kuhusu kuendelea kusalia shuleni kwa wanafunzi .