Mama na wanawe wapatikana wameuawa dukani, mshukiwa akamatwa

Muhtasari
  • Mama na wanawe wawili wauawa na watu Karatina kaunti ya Nyeri
  • Mshukiwa mmoja ametiwa mbaroni ili kuwasaida polisi na uchunguzi zaidi
Pingu
Image: Radio Jambo

Mwanamke mwenye umri wa makamo na wanawe wawili walinyongwa siku ya Alhamisi, Oktoba 23 na watu wasiojulikana ndani ya duka lao katika eneo la Karatina kaunti ya Nyeri.

Walioshuhudia mama huyo akifungua duka lake, walisema ya kwamba mama huyo alifungua duka lake kama kawaida mwendo wa saa tano na kuketi nje ya duka.

Baadaye alipatikana ameaga dunia ndani ya duka hilo na dadake ambaye alikuwa amemtuma mawanawe kununua unga.

 
 

Baada ya kusubiri mwanawe kwa muda na hakurejea nyumbani aliamua kwenda kuangalia kwanini alikuwa amekawia, aligutuka kuona miili ya watu watatu dukani humo akiwepmo mwanawe.

Kamanda wa polisi katika eneo hilo Adiel Nyange alithibitisha kisa hicho na kusema kuwa polisi tayari wameanzisha uchunguzi ili kubaini kiini cha mauaji hayo.

Aliwashauri wananchi wa eneo hilo kutafuta mbinu mbadala za kutatua mizozo baina yao badala ya kuchukua sheria mikononi.

Vile vile aliwaomba wananchi kutoa taarifa zaidi kuhusu tukio hilo ili kuwasaidia polisi kuwasaka washukiwa wa mauaji hayo.

Aida polisi walisema kuwa mmoja wa washukiwa ametiwa mbaroni na anawasaidia polisi katika uchunguzi.

(Mhariri: Davis Ojiambo)