- Rais amesema serikaliz itazidi kuwaunga mkono wahudumu wa boda boda
Rais Uhuru Kenyatta amewashauri wahudumu wa boda boda dhidi ya kutumiwa vibaya na wanasiasa kuafiia malengo yao ya kibinafsi .
Uhuru ameitaja sekta ya boda kama yenye uwezo mkubwa iwapo mikakati itawekwa kutumia vyema michango ya kila siku ya fedha zao .
Amewapa amewarai wahudumu hao kusalia macho ili wasitumiwe vibaya na wanasiasa ambao wanawapa pesa ambazo haziwezi kuwasaidia .
Rais aliyasema hayo siku ya ijumaa wakati alipokutana na muungano wa usalama wa wana boda boda katika Ukumbi wa kijamii wa Pumwani .
Aliongoza kusainiwa kwa mkataba muhimu kati ya Muungano huo BAK , Maamlaka ya mtaji nchini ,Rubis Energy na Nabo Capital .
Amewashauri wahudumu wa boda boda kuwekeza vizuri kutumia kiasi kikubwa cha fedha ambazo wao hupata kila siku lakini kwa kinaya bado wengi wao ni maskini .
Rais alisema sekta ya boda boda ni muhimu sana kwani takriban watu milioni 22 hutumiwa usafiri wa boda boda kila siku .
Uhuru amesema sekta hiyo hupata kiasi cha shilingi bilioni 357 kila mwaka ,kiasi ambacho kinazidi hata mgao unaopewa serikali za kaunti