Raila na Ruto wachimbana makucha Bomas

Raila:Sijatangaza kwamba nitagombea urais 2022

Huwezi kukataa mtoto wako akiwa kichaa-Raila

Muhtasari

 

  •  Raila alisema wakenya wana fursa ya kugeeza dhana  ili kujenga utaifa kwa kujiangazia kama wakenya na sio watu wa makabila  mbali mbali
  • Odinga amesema ripoti ya BBI ilikuwa na lengo la kuhakikisha kwamba kuna usawa miongoni mwa jamii za Kenya bali  haina lengo la kutumiwa kwa  malengo ya kisiasa

 

Kiongozi wa ODM Raila  Odinga amesema Ripoti ya  BBI ni mkusanyiko wa maoni ya wakenya kuhusu taifa wanalotaka lwenye usawa ,upenzo,umoja na mafanikio

 Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti ya BBI  katika ukumbi wa Bomas   Odinga alikanusha ripoti katika vyombo vya hbari kwamba ametangaza kwamba atagombea urais mwaka wa 2022 . Odinga alisema  hajatangaza azma yake kuhusiana na uchaguzi mkuu ujao . Amesema uboreshaji wa katiba ni mchakato wa muda mrefu ambao hufanywa hatua kwa hatua .

 Raila alisema wakenya wana fursa ya kugeeza dhana  ili kujenga utaifa kwa kujiangazia kama wakenya na sio watu wa makabila  mbali mbali

‘Wenzetu  Tanzania  hawaulizani kuhusu makabila yao .sisi pia kama wakenya tunafaa kuanza kujitambua kama wakenya na sio wakisii,wakikuyu waluhya ama wajang’o’ amesema Odinga

 Akionekana kumkosoa naibu wa rais William Ruto kuhusu siasa za mwaka wa 2022, Odinga amesema viongozi wa Jubilee wanafaa kutekeleza ahadi zao wakati huu na sio kungoja hadi mwaka wa 2022 .

‘Viongozi wa Jubilee wako hapa..mbna ungoje hadi mwaka wa 2022…. Huwezi kuwa na mume kisha mkipata mtoto kichaa unasema mtoto sio wako’ Odinga alisema katika usemi ambao uliwachekesha wajumbe katika ukumbi wa Bomas

 Odinga amesema ripoti ya BBI ilikuwa na lengo la kuhakikisha kwamba kuna usawa miongoni mwa jamii za Kenya bali  haina lengo la kutumiwa kwa  malengo ya kisiasa .