Covid 19

14 Wafariki huku visa 836 vya covid 19 vikiripotiwa leo

14 zaidi wafariki

Muhtasari

 

  •  Naironi ina visa 556 
  • 14 wafariki 
Mutahi Kagwe
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe Mutahi Kagwe

 

Kenya siku ya jumanne imesajili visa  vipya 836 vya corona  huku watu 14 zaidi wakiaga dunia kwa ajili ya ugonjwa huo na kufikisha idadi ya walioangamizwa na virusi hivyo kuwa 934 . Idadi ya walioambukizwa sasa imesonga watu 50,833. Watu 618 ni wanaume ilhali wanawake ni 218 .Mgonjwa wa umri wa chini ni mtoto wa miezi minn ilhali wa umri wa juu ana miaka 89

 Idadi hiyo ni kutoka sampuli 4,076 zilizopimwa katika saa 24 zilizopita 

 Habari njema leo ni kwamba watu 403 wamepona  na kufikisha jumla ya idadi ya walipona corona hadi sasa kuwa 34,832

 Kwa sasa watu 1,150 wamelazwa katika hospitali mbali mbali  ilhali 3,961 wapo katika utunzi wa nyumbani.Wagonjwa 38 wapo ICU  ilhali 25 wapo katika kitengo cha HDU .