Mkutano

Binamu yake rais Uhuru aongoza wazee kukutana na Ruto ,Karen

Wazee wa busara

Muhtasari

 

  •  Muigai Amelionya baraza hilo la wazee dhidi ya kuunga mkono mrengo wowote wa kisiasa
  •  Mapema mwezi Oktoba  Muigai   aliyataka makundi ya wazee wa kijamii kuhakikisha kwamba kuna umoja wa kitaifa .

Naibu wa rais William Ruto  amekutana na viongozi wa baraza la kitaifa  la wazee wakiongozwa na mkuu wa baraza hilo  Kung’u Muigai .

  Miongoni mwa waliojiunga na wazee hao ni  mwenyekiti  Phares Rutere

Muigai ni binamu yake rais Uhuru Kenyatta .Maajuzi Migai amewashtumu wazee wa jamii ya Kikuyu ambao walisafiri hadi Bondo kwa mkutano katika boma la kiongozi wa ODM Raila Odinga . Amelionya baraza hilo la wazee dhidi ya kuunga mkono mrengo wowote wa kisiasa

 

 Mapema mwezi Oktoba  Muigai   aliyataka makundi ya wazee wa kijamii kuhakikisha kwamba kuna umoja wa kitaifa .

  “ Kama wazee hatufai kujiingiza katika siasa ndogo ndogo .Msimamo wetu ni kwamba  Viongozi wote wa kisiasa ni watoto wetu  na ukiwapata watoto wako wakipigana,je utachukua kiboko na kuanza kumchapa mmoja wao?’ alihoji .

 Wakati wa mkutano wa Karen na Ruto  ,naibu wa rais alisema kwamba wazee wanafaa kuwa mstari wa mbele kuleta umoja  na kumaliza ukabila nchini .

 Ruto amesema wazee wakihusika na mchakato mzima wa kuleta utangamano  basi Kenya itaafikia maendeleo yafaayo na kuwa na  Amani