- Wakilishi watatu wapatikana na corona
- Bunge lilifaa kurejelea vikao vyake jumatatu
- waakilishi wa kaunti walioambukziwa kujitenga
Taharuki imetanda katika bunge la kaunti ya Mombasa baada ya wakilishi watatu wa wadi kupatikana na virusi vya corona . Likizo ya wiki mbili ya viongozi hao sasa imongezwa kwa siku 14 zaidi .wakilishi hao walifaa kurejea kazini siku ya jumatatu .Naibu spika Fadhili Makarani alithibitisha maambukizi hayo na kusema kwamba siku hizo 14 zinaweza kuzidishwa kuwa 21 .
“ Tuna wakilishi watatu wa wadi ambao wameptikana na virusi vya corona ndio kwa sbaabu tumeamua kuzidisha muda wa likizo kwa wiki mbili ili wajiteng’ amesema Makarani .
Wakilishi wa kaunti sasa wapo hatarini kwani walifichwa kuhusu maambukizi hayo kwa sababu zoezi la kuwapima lilikomeshwa kwa ajili ya gharama yake ya ‘juu’
Makarani hata hivyo amesema kuna wafanyikazi ambao wapo kazini na watahitaji kupimwa .
Amesem,a kwa sababu ya unyanyapaa unaomatana na watu kupatikana na ugonjwa huo waliamua kutotoa maelezo hayo kwa njia ambayo ingzua hofu miongoni mwa wafanyikazi wa kaunti . Amesema uongozi wa bunge la kaunti hiyo utachukua hatua za kuhakikisha kwamba kila mtu anapimwa .