Sudan sasa kufanya biashara na kampuni za Amerika
Serikali ya Marekani siku ya jumatatu imeondolea Sudan vikwazo vya muda wa miaka 23 baada ya nchi hiyo kupa akutounga mkono vitendo vya kigaidi siku zijazo .
Rais Donald Trump kupitia taarifa amesema hatua hiyo imechukuliwa baada ya Sudan kukubali kutoa fidia ya Dola milioni 335 kwa waathiriwa wa mashambulizi ya kigaidi . Vikwazo hivyo vimeizuia Sudan kufanya biashara yoyote kutumia sarafu ya dola au kununua bidhaa za kutoka Marekani .
Hatua hiyo ilimaanisha kwamba hakuna kampuni za Amerika zilizotaka kufanya biashara na Sudan kwa kipindi hicho hali ambayo ilichangia kuzorotesha uchumi wa nchi hiyo huku mashirika ya serikali kama vile ye ndege na viwanda vikikosa kununua vifaa na kupewa huduma za ukaraat na biashara za Marekani na washirika wake .
Baada ya kuafikiwa makubaliano hayo ,Sudan sasa ipo huru kufanya mikataba na kampuni za Marekani na mataifa mengine ya magharibi kwa mara ya kwanza tangia mwaka wa 1997 wakati vikwazo hivyo vilipotangazwa