- 16 wameaga dunia leo
- Watu 1018 wamepatikana na virusi vya corona
Watu 1018 wamepatikana na virusi vya corona baada ya sampuli 6,649 kupimwa katika saa 24 zilizopita . Idadi hiyo inafikisha 51,851 idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini na jumla ya sampuli zilizopimwa sasa ni 672,771. Kutoka visa hivyo 989 ni vya wakenya ilhali 29 ni raia wa kigeni .mgonjwa wa umri wa chini ni mtoto wa miezi 9 ilhali wa umri wa juu ana miaka 96 .
Leo watu 426 wamepona ugonjwa huo na kufikisha 35,258 idadi ya jumla ya walipona hadi sasa
Hata hivyo watu 16 wameaga dunia na kufikisha 950 idadi ya walioangamizwa na virusi hivyo hadi sasa.
Wagonjwa 1060 wamelazwa katika hopitali mbali mbali nchini ilhali 4,230 wapo katika mpango wa utunzi nyumbani . wagonjwa 36 wapo katika kitengo cha ICU45 Wagonjwa 1060 wamelazwa katika hopitali mbali mbali nchini ilhali 4,230 wapo katika mpango wa utunzi nyumbani . wagonjwa 36 wapo katika kitengo cha ICU ilhali 45 wanasaidia kupumua na mashine