- Kaunti za Makueni na Kakamega zafurahia sana ugatuzi
- Tana River na Taita Taveta zasema hazijafurahia ugatuzi
Asilimia 73 ya wakenya wanahisi kwamba ugatuzi umeleta mabadiliko katika maeneo ya mashinani ikilinganishwa na kabla ya kuanza kwa mfumo huo wa utawala . Kwa mujibu wa utafiti wa kura ya maoni uliofanywa na kampuni ya Infotrak asilimia 15 ya waknya hata hivyo wanasema hali imekuwa mbaya Zaidi kuliko hapo awali ilhali asilimia 12 wanasema hapajakuwa na mabadiliko yoyote .
Wakaazi wengi wa kaunti za Makueni na Kakamega kwa asilimia 90 ndio wanaosema kwamba kumekuwa na mabadiliko makubwa sana yaliyosababishwa na ugatuzi .
Kaunti nyingine zinazofurahia ugatuzi ni Turkana na West Pokot kwa kwa asilimia 87, Machakos kwa asilimia 86 , Kericho kwa asilimia 82 ,Mandera Bomet ,kisumu na Uasin Gishu kwa asilimia 81 na Elgeyo Marakwet na Kisii kwa asilimia 80 .
Kaunti ambazo wakaazi hajawaona tofauti ni Taita Taveta kwa asilimia 48, Tana River kwa asilimia 56 ,Kiambu kwa asilimia 56 ,Homabay kwa asilimia 57 na Trans Nzoia kwa asilimia 58 .
Jumla ya watu 37,600 kote nchini walihojiwa katika utafiti huo wenye uhakika wa asilimia 95