Muhtasari
- Mahakama kuu ilikuwa imesema hakuchaguliwa kwa njia ifaayo
- Sasa uamuzi wa jaji Korir umesimamishwa hadi rufaa iamuliwe
Mahakama ya rufaa imefutilia mbali uamuzi wa mahakama kuu uliokuwa umetupilia mbali uchaguzi wa mbunge wa gatundu Kaskazini Anne Wanjiku .
Wanjiku kupitia wakili wake Tom Ojienda alikuwa amewasilisha rufaa akisema hakuridhishwa na uamuzi uliotolewa na jaji Weldon Korir ambaye alikitangaza kiti chake kuwa wazi .
Mnamo oktob tarehe 7 Jaji Korir alisema kwamba Wanjiku hakuwa amechaguliwa kwa njia ifaayo kwani wakati huo alikuwa yungali akihudumu kama mwakilishi wa kaunti .
Majaji Martha Koome , Daniel Musinga na Sankale Ole Kantai wamesimamisha uamuzi wa Korir hadi uamuzi wa rufaa hiyo utolewe .