Heroin yanaswa

KRA yanasa Heroin na bangi katika uwanja wa JKIA

Bangi pia ilinaswa

Muhtasari

 

  •  kumekuwa na ongezeko la visa vya usafirishaji wa dawa za kulevya kupitia JKIA

 

Halmashauri ya ukusayaji ushuru nchini KRA imenasa  Heroin na bangi  ambayo ilikuwa ikisafirishwa kupitia uwanja wa ndege wa JKIA .

 Dawa hiyo ya  heroin ilikuwa ikisafirishwa kutoka Juba ,Sudan kusini  na ilikuwa ikipelekwa Cambodia  ilhali bangi ilikuwa ikitoka kasese nchini Uganda ikipelekwa nchini ufaransa .

 Shehena zote za dawa hizo za kulevya  ziligunduliwa wakati wa ukaghuzi katika mashine maalum kwenye uwanja huo wa ndege . Dawa ya heroin ilikuwa imefichwa katika mafungu ya nguo ilhali bangi ilikuwa imefichwa katika mfuko mweusi wa plastiki na kuwekwa ndanio ya nguo ya kitenge .

 Wiki moja iliyopita  shehena nyingine ya heroine iliyokuwa imefichwa katika mafungo ya nguo ilinaswa ikitoka Juba kupelekwa  ufaransa na Cambodia  kupitia uwanja wa JKIA .