Hatari

Makao makuu ya kaunti ya Kakamega yafungwa huku visa vya corona vikizidi

Kaunti kadhaa zimeanza kufunga afisi zake

Muhtasari

 

  •  Oparanya achukua hatua baada ya visa kuongezeka
  • Serikali kuu pia inahofishwa na ongezeko la idadi ya waliombukizwa 

 

Gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya

 Makao makuu ya kaunti ya kakamega yamefungwa kwa wiki moja  kufuatia ongezeko la visa vya corona  katika siku za hivi karibuni .

Gavana  Wycliffe Oparanya  ametangaza siku ya jumatano  kusitishwa kwa shughuli zote katika afisi za makao makuu ya kaunti na kuagiza kwamba wafanyikazi wote wapimwe ugonjwa huo .

 Hatua hiyo inajiri siku moja tu baada ya bunge la kaunti hiyo kusitisha shughuli zake  kwa wiki mbili baada ya wakilishi watatu wa wadi kupatikana na virusi vya corona .

 Kaunti hiyo ina jumla ya visa 316 vya corona  huku 57 vikiwa vya wahudumu wa afya  . idadi hiyo ndio ya juu Zaidi  tangu kisa cha kwanza kuripotiwa nchini mwezi machi .

 Miongoni mwa walioathiriwa ni  maafisa wakuu katika ofisi ya oparanya .Gavana huyo amesema watu saba wameaga dunia katika kaunti ya kakamega kwa ajili ya virusi hivyo .

Oparanya  amesema utunzi wa nyumbani sasa utaboreshwa kwa wote walio na virusi hivyo ili kuepuka mrundiko wa watu katika vituo vya  afya . Hospitali nyingi za kakamega zimezidiwa na idadi ya juu ya wagonjwa huku visa zaidi vikiripotiwa kila siku . Wiki ijayo rais Uhuru kenyatta ataanda mkutano na magavana ili kujadili hatua Zaidi za kuchukuliwa kukabiliana na ongezeko la maambukizi ya ugonjwa huo nchini .