- Hatma yake sasa ipo mikononi mwa bunge
- Rais alimteu wiki jana kuhudumu kama kamishna wa Data
Maamuzi aliofanya Immaculate Kassait wakati wa uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali wa mwaka wa 2017 yamerejea kumsakama wakati akihojiwa kuwa kamishna wa data alipofika mbele ya wabunge siku ya jumatano
Kassait ambaye amekuwa mkurugenzi wa IEBC wa elimu kwa wapiga kura kabla ya kuteuliwa na rais Kenyatta kuwa kamishna wa Data amejipata na kibarua kikubwa cha kueleza mbona anafaa kupewa kazi hiyo kwa ajili ya mzigo wa maamuzi ambayo yalitiliwa shaka wakati wa uchaguzi mkuu wa 2017 ambapo tume hiyo ilikataa kutii uamuzi wa mahakama ya juu Zaidi kufungua sava zake ili kubaini mshindi halisi wa uchaguzi wa urais .
Mbunge wa Mathare Anthony Oluoch alimpa kibarua Kassait kueleza jinsi atakavyorejesha Imani ya wakenya kwake kufuatia matuko ya 2017 . Oluoch amesema wakenya wengi hawana Imani na IEBC ,taasisi ambayo Kassait alikuwa miongoni mwa viongozi wake .
Kassait kwa upande wake alisema atahakikisha kwamba data ya wakenya inahifadhiwa kwa njia salama na kulindwa ili kutotumiwa vibaya na yeyote .
Afisi ya kamishna wa data ina jukumu kubwa la kuhifadhi sajili na maelezo ya wakenya pamoja na kuchunguza visa vya utumizi mbaya wa data .
Kassait aliteuliwa kuhudumu katika nafasi hiyo na rais Uhuru Kenyatta wiki jana na uteuzi wake utaidhinishwa iwapo wabunge watakubaliana na rais . Spika Justin Muturi aliipa kamati ya bunge kuhusu mawasiliano jukumu la kumhoji Kassait kabla ya kuwasilisha ripoti yake bungeni