- Utafiti watambua kaunti zenye utendaji kazi bora
- Kisumu , Uasin Gishu na Elgeyo Marakwet zipo katika tano bora
Kaunti za Kakamega ,Kwale na Makueni zinaongoza ktika utendakazi kwa mujibu wa utafiti wa kura ya maoni ilioyofanywa na kampuni ya infotrak . Asilimia 57.2,54.8 na 54.4 ya wakaazi wa kaunti hizo mtawalia walionyesha kuridhika na utendakazi na utoaji huduma wa kaunti hizo tatu
Kaunti nyingine zenye utendakazi wa juu kwa mujibu wa wakaazi wake ni Kisumu kwa asilimia 53.4,Uasin Gishu kwa asilimia 53.1 ,West Pokot kwa asilimia 52.7 na Elgeyo Marakwet kwa asilimia 51.2
Kaunti zinazoshika mkia kwa utendakazi ni Tana River kwa asilimia 39.5,Wajir kwa asilimia 41.3,Isiolo kwa asilimia 42,samburu kwa asilimia 42.2,mandera kwa asilimia 43.1 na Trans Nzoia kwa asilimia 43.4
Katika utafiti huo uliohusiha jumla ya watu 37,600 kote nchini Nyeri ndio kaunti yenye utendakazi bora katika kaunti za Eneo la kati kisha Kiambu ni ya mwisho . Kwale inaongoza kwa kaunti za pwani nayo Tana River ni ya mwisho . Makueni inaongoza kwa kaunti za eneo la Mashariki huku Isiolo ikishika mkia . Garissa inaongoza kwa kaunti za kaskazini mashariki ,Kisumu inaongoza kwa kaunti za Nyanza ,Uasin Gishu inaongoza kwa kaunti za Rift valley Ilhali Kakamega ndio inayoongoza kwa kaunti za Magharibi huku Busia ikishika mkia kwa utendakazi