Siasa na sanaa

Willy Paul akutana na DP Ruto, Kuna mazuri?

Ruto amewavutia wasanii kadhaa upande wake kabla ya 2022

Muhtasari

 

  •  Willy Paul  amekutana na DP Ruto ,kwake Karen 

 

  Wakati wa Siasa  wasanii wengi hujipata katika kambi mbali mbali za viongozi ambao hushindania nafasi za uongozi .

Miaka miwili kabla ya uchaguzi mkuu ujao ,mambo sio tofautio kwani siasa na Sanaa hukutana na Naibu wa rais William Ruto amekuwa mweledi sana wa kuwavutia wasanii kwa upande wake 

 Orodha ya wasanii ambao DP amejinyakulia katika harakati zake za kuchukua uongozi wa nchi ni ndefu  na wa hivi punde kukutana na Ruto ni msanii Willy Paul .

 

 Dp Ruto alithibitisha mkutano huo kwa picha alizoweka kwenye twitter akisema yeye na  Willy Paul jina halisi Wilson Radido walikubaliana kushirikiana ili kuendeleza Sanaa