Idadi ya visa vya corona inazidi kuongezeka

14 wafariki huku 761 wakipatikana na virusi vya corona

Kagwe asema awamu ya pili ya janga la corona imeanza

Muhtasari
  •  Watu 14 wamefariki leo 
  • watu 761 wamepatikana na corona siku ya alhamisi 

 

Mutahi Kagwe
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe Mutahi Kagwe

Kenya siku ya alhamisi imesajili visa vipya 761 vya corona baada ya watu 4830 kupimwa  katika saa24 zilizopita.

  Idadi hiyo sasa inafikisha jumla ya visa vya corona nchini kuwa 52,612  na idadi ya sampuli zilizopimwa ni 678,000.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema watu wengine 14 wameaga dunia kwa ajili ya corona na kufikisha jumla ya vifo  vilivyotokana na ugonjwa wa corona kuwa 964 .

 

Watu wengine  1084 wamelazwa hospitalini  huku 35 wakiwa katika kitengo cha ICU .

 Kagwe amesema  kuanzia sasa watu wanaopatikana na corona watakiwa wakitibiwa nyumbani na sio hospitalini .Kagwe amesema familia zitalazimika kuwahudumia na kuwatunza jamaa zao ambao wanapatikana na virusi vya corona .

  Kiwango cha maambukizi sasa ni asilimia 15 . Kagwe amesema maambukizi yanafanyika katika maeneo yalio na watu wengi kama sehemu za burudani .

 Kagwe amewahimiza wakenya kuendelea kufuata kanuni zilizotolewa  na wizara ya afya kama vile kuvalia maski  na kuepuka maeneo ya watu wengi ili kuzuia usambaaji wa virusi vya corona .