Utata

Bilioni 14? Hapana! Raila aiambia IEBC kuhusu gharama ya kura ya maoni

Gharama ya kura ya maoni yazua mzozo

Muhtasari

 

  •  Odinga asema wakenya hawafai kugharamika zaidi kuandaa kura ya maoni 
  • Adai  uchaguzi uekuwa ukitumiwa kuwapunja fedha wakenya 
  • Asema IEBC  inafaa kutumia shilingi bilioni 12 kuandaa kura ya maoni 

 

Kiongozi wa ODM Raila odinga

 Tume huru ya uchaguzi na mipaka  inafaa kurekebishwa na uongozi wake kubadilishwa  baada ya  kudai kwamba kura ya maoni itahitaji shilingi bilioni 14 ,amesema kiongozi wa ODM Raila Odinga

 IEBC siku ya jumanne ilisema kwamba kura ya maoni ili kuirekebisha katiba itahitaji shilingi bilioni 14  ,kiasi ambacho Odinga amesema ni cha juu zaidi .

 Gharama hiyo imetegemea idadi ya wapiga kura milioni 19.6 ,idadi ambayo huenda itapanda kwa sababu ya  kuendelea kwa zoezi la kuwasajili wapiga kura katika kaunti zote 47 .

" Katika muda mfupi ujao tutaunda kundi la kujadili na IEBC ili kuunda orodha ya vitu vyote vinavyohitajika ili kuandaa kura ya maoni ya gharama inayiokubalika’amesema Raila .

Kupitia taarifa siku ya alhamisi  Raila amesema uchaguzi umekuwa ukitumiwa mara nyingi kama  njia ya kupunja fedha za walipa ushuru .

" Njama hizi zipo wazi kutokana na jinsi IEBC Inavyofikiria . ukiukaji huo wa sheria haufai kuendelea katika nchi yetu  katika zoezi muhimu lijalo la kura ya maoni kuhusu ripoti ya BBI ‘Amesema Raila .

Raila  amesema kura ya maoni ililenga  kuleta unadhifu katika mchakato wa uchaguzi nchini  ikiwemo kuainisha gharama za uchaguzi na  viwango vya nchi nyingine duniani .

" Ujumbe huo unafaa kuifikia IEBC. Gharama kwa kila mpiga kura inafaa kuwa kati ya shilingi 100 hadi 200 . hakuna sababu yam bona wakenya wanafaa kulipa zaidi’

 Odinga ameshikilia kwamba kura ya maoni haifai kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 2 kwa wapiga kura milioni 20 .

" Kiasi cha pesa ambacho IEBC inazungumzia ni cha juu zaidi na hil linashangaza  na pia ni daalili kwamba baadhi ya mashirika ya umma hayajali kuhusu kilio cha wakenya  kutokana na jinsi yanavyosimamia masuala ya umma’Amesema Raila .