Uhasama

Murathe akosoa ziara ya Ruto kwenda eneo la Mlima Kenya

Murathe asema wakaazi wa Mlima kenya wawe waangalifu na DP Ruto

Muhtasari

 

  •  Ruto anategemea ngome ya rais Uhuru mwaka wa 2022 
  • Washirika wake wanatarajiwa kujibu baadahi ya matamshi ya Viongozi wanaompinga Ruto 
  •  Ruto amefanya ziara nyingi katika eneo la Mlima Kenya 
David Murathe
David Murathe David Murathe

Naibu mwenyekiti wa chama cha Jubilee  amehoji  ziara za kila mara za naibu wa rais   William Ruto  huku ya hivi  punde ikiwa kwenda katika eneo la Mlima Kenya .

Murathe,  ambaye hapatani na Ruto amesema ziara hizo zinazua maswali mengi kuliko majibu .

 Huku akisema Ruto ana haki ya kuzuru eneo lolote la nchi  ,Murathe amesema Ruto ana hila kwa ajili ya ziara zake kwenda katika eneo la mlima Kenya  na amewatahadharisha wakaazi wa eneo hilo kuwa makini .

 “ Tunahisi kwamba Ruto yupo katika kampeni ya kuwachochea watu na tunawapa tahadhari watu wentu kuwa wangalifu’amesema Murathe

 “ Tulikuwa na tatizo la mungiki katika eneo la kati …sasa ukileta huu mjadala wa walio navyo na wasio navyo …hiyo ndio iliyokuwa  kauli mbiu ya Mungiki’

 Pia amekosoa mpango wa wa Ruto wa kuwahamaisha vijana na wanawake  kiuchumi  ,akisema kwamba  mpango huo unafaa pia kufanywa katika eneo la Rift valley .

 Murathe pia amedai kwamba ziara ya Ruto katika eneo la mlima Kenya imekuwa na ubaguzi  Fulani kwani amekuwa akiandamana na wajumbe kutoka maeneo bunge mengine .

“ Iwapo ni jambo litakalowafaidisha  vijana na wanawake wetu mbona usiende na uongozi wa maeneo bunge husika?’

Ruto wikendi hii atazidi kufanya ziara zake katika eneo la mlima Kenya  ,ambalo ndio ngome ya rais Uhuru Kenyatta .

 Amepanga msururu wa mikutano katika kaunti za Murang'a, Kirinyaga, Nyeri, Tharaka Nithi  kuanzia siku ya ijumaa hadi jumapili .

 Ziara hizo zinakuja baada ya kuzinduliwa kwa ripoti ya BBI  ambapo uhuru alimtaja Ruto kama msaidizi asiye na subira  ,washirika wa Ruto watajaribu kupunguza makali ya rais . Kenyatta alisema Ruto aliacha ajenda ya Jubilee na kuanza kuzingatia kampeini za uchaguzi wa mwaka wa 2022.