- Sumbi alihamishwa hadi Bungoma ili baada ya hali yake kudhoofika
- Oparanya amemtaja kama mchapa kazi na rafiki yake wa karibu
Gavana wa kakamega Wycliffe Oparanya ameomboleza kifo cha afisa mkuu wa wafanyikazi katika kaunti hiyo aliyekuwa akiugua virusi vya corona .
Robert Sumbi aliaga dunia siku ya alhamisi katika hospitali ya Life Care mjini Bungoma ambako alikuwa amehamishwa kutoka hospitali ya kaunti ya kakamega baada ya hali yake kuzoto siku ya jumatano .
Ni miongoni mwa maafisa wakuu wa kaunti waliopata ugonjwa huo katika siku za hivi karibuni
"Sumbi alikuwa mtu aliyejitolea ,mchapa kazi ,mtu mkweli na aliyekuwa mchango mkubwa sana ‘amesema Oparanya
Kupitia taarifa ,oparanya amesema kifo cha Sumbi ni pigo kubwa kwa serikali ya kaunti ya kakamega
" Tumempoteza mtu aliyekuwa na maono na ambaye mchango wake utakosekana sana . nimempoteza rafiki na mshirika wa karibu ambaye ushauri na msaada wake ulinisaidia katika kufanya maamuzi muhimu’amesema Oparanya .
Sumbi alifaa kufanyiwa dialysis kwa ajili alikuwa na maradhi ya figo na hangeweza kuhudumiwa katika hospitali kuu kwa sababu ya kuwa na virusi vya corona .
" Tulilazimika kumhamisha hadi Bungoma kwani wangeweza kumfantyia dialysis na kumweka katika kitengo cha ICU kwa sababu vitanda vyetu vya ICU hapa vina wagonjwa wengine wa corona’amesema daktari mmoja
Sumbi alihudumu kama waziri wa kaunti wa mazingira na maji kati ya mwaka wa 2013 na 2017 .Alitajwa kuwa mkuu wa utumishi wa wafanyikazi baada ya Oparanya kuchaguliwa tena mwaka wa 2017