- Moderna imepokrea zaidi ya dola bilioni 1 za kufanya utafiti kutoka kwa serikali ya Marekani na ina mkataba wa dola bilioni1.5 kutoa dozi milioni 100 za chanjo yake
- Kampuni hiyo sasa imesema itatafuta idhini ili kuruhusiwa kutumia chanjo hiyo kupambana na virusi vya corona
Kampuni ya kutengeza dawa ya Moderna Inc imesema jumatatu kwamba chanjo yake dhidi ya corona ina uwezo wa asilimia 94.5% kuzuia virusi vya corona na kuwa kampuni ya pili ya Marekani katika kipindi cha wiki moja kutoa matokeo yanayozidi matarajio
Kampuni hiyo sasa imesema itatafuta idhini ili kuruhusiwa kutumia chanjo hiyo kupambana na virusi vya corona
Tathmini ya kwanza ya matumizi ya chanjo hiyo imetokana na na visa 95 vya corona
Matokeo hayo yametolewa wiki moja baada ya kampuni ya Pfizer Inc na mshirika wake wa ujerumani BioNTech SE kusema kwamba chanjo yao ilikuwa na uwezo wa Zaidi ya asilimia 90 kuzuia corona .
Moderna, ambayo ilianza kutambulika mwaka wa 2018 imepokrea zaidi ya dola bilioni 1 za kufanya utafiti kutoka kwa serikali ya Marekani na ina mkataba wa dola bilioni1.5 kutoa dozi milioni 100 za chanjo yake . Serikali ya Marekani ina chaguo la kuitisha dozi nyingine milioni 400 na Moderna pia ina mikataba nan chi nyingine kutoa chanjo hiyo