Tshala Muana akamatwa

Mwanamuziki wa Congo Tshala Muana akamatwa kwa ajili ya wimbo wake mpya

msanii huyo anafahamika kwa nyimbo zake kote Afrika

Mwanamuziki wa Congo Tshala Muana amekamatwa na shirika la ujasusi la DRC kwa ajili ya wimbo wake mpya kwa jina Ingratitude unaoonekana kumkosoa rais wa sasa Felix Tshisekedi .

Producer wake  Claude Mashala amethibitisha kukamatwa kwa mwanamuziki huyo  kwa ajili ya maudhui ya wimbo wake ambao haujawapendeza baadhi ya maafisa wakuu serikalini . Wimbo huo unamkosoa mtu ambaye aliwasaliti watangulizi wake ukionekana kuashiria uhusiano mbaya wa sasa kati ya rais Tshisekedi na  mtanguzi wake Joseph Kabila .

 Mwanamuziki  mwenzake  Lofombo Gode amesema ingawaje hakuna majina yaliotajwa atika wimbo huo ,inadaiwa una maana ya ndani ambayo haijawafurahisha wafuasi wa rais wa sasa .

 Jamaa za mwanamuziki huyo maarufu wamesema alichukuliwa na maafisa wa ANR ili kuhojiwa na wamelalamika kuhusu alivyokamatwa .

 Msanii huyo mwenye umri wa miaka 62 ni mfuasi wa rais wa zamani Joseph Kabila kwani awali aliwahi kuteuliwa kuwa mbunge na  babake rais huyo marehemu  Laurent Kabila .

 Katika wimbo wa Tshala Muana ,waliofaulu kuunganoisha maana yake na hali ya sasa ya kisiasa wanasema ,anayelaumiwa kwa kuwasaliti watangulizi wake ni rais Tshisekedi ambaye Kabila alimsaidia kutengeza muungano wa kuunda serikali yake lakini kwa muda sasa uhusiano katika muungano huo haujakuwa mzuri na kuzua taharuki katika taifa hilo .

 Wafuasi wa  Tshisekedi,  kwa sasa hawapatani na kambi ya  Kabila na wimbo huo unaonekana kumlenga rais .

 Serikali haijatoa maelezo kuhusu kukamatwa kwa Tshala Muana lakini imepiga marufuku kuchezwa kwa wimbo huo katika vituo vya redio