Leta pesa zangu

Karua awatuma madalali kuchukua shilingi zake milioni 6.5 kwa Moses Kuria

Kuria aliagizwa na mahakama kumlipa Karua fedha hizo

Muhtasari

 

  •  Karua amewatuma madalali kuuza mali ya Kuaria ili  azipate fedha hizo 
  •  Hatua hiyo inatokana na agizo la mahakama kuhusu kesi ambayo Kuria alipatikana na hata ya kumharibia jina kiongozi huyo wa Narc Kenya 

 

Kiongozi wa Narc -Kenya Martha Karua amewatuma madalali kuuuza kutwaa ali ya mbunge wa Gatundu kusini Moses Kuria ili kujipa shilingi zake milioni 6.5  ambazo mahakama ilimuagiza Kuria amlipe mwaka wa 2017

 Kuria alikuwa ameagizwa na mahakama kumlpa Karia fedha hizo kwa ajili ya kesi ya kumchafulia jina .Mahakama kuu  ilitoa uamuzi huo katika kesi ambayo Kuria alidai kwamba Karua aliwatafuta mashahidi wa kutumiwa dhidi ya  naibu wa rais William Ruto katika kesi yake ya ICC

 Katika barua ambayo gazeti la The Star imeoina  Karua amewatuma madalali  kuuza bidhaa za nyumba  kama vile viti vya sofa ,meza ,runinga na magari mawili ya Kuria ili aweze kujilipa pesa hizo .

 Mwaka wa 2017 Karia aliitisha shilingi milioni 20 kutoka kwa mbunge huyo kwa kumharibia jina kupitia matamshi hayo yake . Amesema licha ya kumtaka Kuria aombe msamaha  alienda bungeni na kurudia kutoa matamshi hayo

 

FILE_1575031167__1577790071_92124
Moses Kuria FILE_1575031167__1577790071_92124