Sakata ya Marehemu

Mahakama yazuia kuzikwa kwa mbunge Murunga baada ya pingamizi ya ‘mpenzi’ wake

Agnes Wangui anasema ana watoto wawili na Murunga

Muhtasari

 

  •  Anataka kuhusishwa na mipango ya mazishi ya Murunga 
  •  Amesema amepata watoto wawili na mbunge huyo 

 

Marehemu Justus Murunga

  Mahakama imetoa agizo la kuwazuia  wajane wawili  wa mbunge wa Matungu Justus Murunga dhidi ya kuanda mazishi yake .

 Hakimu wa mahakama ya milimani  Agnes Makau  siku ya alhamisi  ametoa  agizo hilo na kuelekeza kwamba Agnes Wangui   anayedai kuwa mpenzi wa mbunge huyo  awakabidhi wajane hao na chumba cha kuhifadhi maiti cha Lee stakabadhi za mahakama kuhusu kesi hiyo itakayoikizwa tarehe 26 mwezi Novemba

Wangui  kupitia wakili wake Danstan Omari  aliwataka wajane hao wawili  Chritabel na Grace pamoja na hifadhi ya maiti ya Lee kuzuiwa kuandaa mazishi ya mbunge huyo .

 Pia anataka kuchukuliwa kwa sampuli ya DNA ili kubainisha kwamba Marehemu Murunga ndiye baba ya watoto wake wawili .  Anataka mwili wa Murunga kuhifadhiliwa Lee hadi  sampuli hizo zichukuliwe

Wangui,  kupitia waraka maalum kwa mahakama amesema watoto wake wawili ni wa marehemu Murunga .  Amesema kwamba anahofia wajane wa mbunge huyo watamuacha nje ya mipango ya mazishi ya Murunga .

Kupitia waraka kwa mahakama amesema amemjua mbunge huyo kwa mika saba tangu mwaka wa 2013  alipokuwa msimamizi katika shamba la Embakasi   na  yeye alipokuwa mfanyibiashara  katika eneo la Ruai .

 Agnes amesema baada ya kuanza kwa uhusiano wao wa kimapenzi na kuwapata watoto wawili  ,Murunga alimkodishia nyumba katika mta wa Ruai.Uhusiano wao ulianza kuvurugika mwaka wa 2017 baada ya mbunge huyo kushinda kiti cha ubunge cha Matungu