Corona

19 waaga dunia huku 1,048 wakipatikana na Corona

Watu 19 wameaga dunia leo

Muhtasari

 

  • Watu 1,048 wamepatikana na virusi vya corona siku ya ijumaa 
  • Leo watu 326 wamepona na kufikisha 50,984 idadi ya watu waliopona ugonjwa huo hadi kufikia sasa .

 

Mutahi Kagwe
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe Mutahi Kagwe

 Watu 1,048 wamepatikana na virusi vya corona baada ya sampuli 8,660 kupimwa katika saa 24 zilizopita na kufikisha 75,193 jumla ya visa hivyo nchini huku sampuli zilizopimwa zikiwa 823,700 . Kutoka visa hivyo 1,018 ni wakenya ilhali 30 ni raia wa kigeni  .watu 594 ni wanaume ilhali 454 ni wanawake .Mgonjwa wa umri wa chini ni mtoto wa mwaka mmoja ilhali wa umri wa juu ana miaka 90

Leo watu 326 wamepona na kufikisha 50,984 idadi ya watu waliopona ugonjwa huo hadi kufikia sasa .

 Hata hivyo watu 19 wameaga dunia na kufikisha  1,349 idadi ya watu waliofariki  kwa ajili ya corona .

 Kuna wagonjwa 1,114 waliolazwa katika hospitali mbali mbali  nchini huku  wngine 6,332  wakiwa chini ya utunzi wa nyumbani . wagopnjwa 52 wapo katika kitengo cha ICU