Uchaguzi Uganda

Bobi Wine ashtakiwa kwa ‘kusambaza corona’

Maandamano yamesababisha vifo vya watu takriban 29

Muhtasari

 

  •  Maandamano yalizuka pindi Wine alipokamatwa siku ya jumatano na kusababisha vifo vya watu takriban 29 
  • Kukamatwa kwake kumedaiwa kutokana na hatua yake yake kukiuka kanuni za covid 19 kwa kuruhusu watu wengi kuliko inavyokubalika kukongamana katika sehemu moja .

 

Bobi Wine

Mgombeaji wa urais nchini Uganda Bobi Wine ameshtakiwa kwa ‘kusambaza corona’ na kuachiliwa kwa dhamana

 Mahakama imeamuru kwamba Wine mwenye umri wa miaka 38 aliandaa mktano uliowaleta pamoja watu wengi kinyume na kanuni za kuzuia usambaaji wa virusi hivyo . mashirika  ya kutetea haki za binadamu yamedai kwamba serikali nchini humo inatumia corona kama kisingizo cha kuwakandamiza viongozi wa upinzani na wafuasi wao .

 Maandamano yalizuka pindi Wine alipokamatwa siku ya jumatano na kusababisha vifo vya watu takriban 29  . msanii huyo ambaye jina halisi ni  Robert Kyagulanyi,  ni miongoni mwa wagombeaji 11 wa urais wanaotaka kumuondoa madarakani rais Yoweri museveni ambaye ameiongoza  nchi hiyo tangu mwaka wa 1986  

Kukamatwa kwake kumedaiwa kutokana na hatua yake yake kukiuka kanuni za covid 19 kwa kuruhusu watu wengi kuliko inavyokubalika kukongamana katika sehemu moja .Maandamano yalioafutia yamesababisha kuuawa kwa watu 16 lakini duru nchini humo zinasema idadi hiyo ni ya juu kuliko inavyotangazwa .

 “ Kuongezeka kwa ghasia na machafuko kabla ya uchaguzi sio ishara nzuri’ amesema   mtafiti wa Afrika  Oryem Nyeko

 Katika wiki mbili  zilizopita  ,maamlaka zimewakamata viongozi wa upinzani ,wanahabari na kuwatawanya wafuasi wa upinzani  kwa madai ya kujikusanya kinyume na kanuni za Covi 19