- Polisi hata hivyo wamekuwa wakiwaruhusu wafuasi wa chama tawala NRM kukongamana bila kuwatawanya
- Mamia ya watu wamejeruhiwa katika makabiliano ya wafuasi wa upinzani na polisi tangu kukamatwa kwa Bobi Wine
Kukamatwa na kuzuiliwa kwa mgombeaji wa urais wa Uganda Robert Kyagulanyi, ni ishara ya kukandamizwa kwa upinzani nchini humo ,shirika la Human Rights Watch limesema .uchaguzi nchii uganda utandaliwa januari mwakani .
Kupitia taarifa siku ya ijumma HRW limeitaka mamlaka nchini humo kumuachilia Kyagulanyi mara moja na bila masharti na kuheshimu haki za binadamu za wananchi
Kyagulanyi, anayaefahamika kwa jina la usanii kama Bobi Wine alikamatwa siku ya jumatno katika mkutano wa kampeni wilayani Luuka .
Kukamatwa kwake kumedaia kutokana na hatua yake yake kukiuka kanuni za covid 19 kwa kuruhusu watu wengi kuliko inavyokubalika kukongamana katika sehemu moja .Maandamano yalioafutia yamesababisha kuuawa kwa watu 16 lakini duru nchini humo zinasema idadi hiyo ni ya juu kuliko inavyotangazwa .
“ Kuongezeka kwa ghasia na machafuko kabla ya uchaguzi sio ishara nzuri’ amesema mtafiti wa Afrika Oryem Nyeko
Katika wiki mbili zilizopita ,maamlaka zimewakamata viongozi wa upinzani ,wanahabari na kuwatawanya wafuasi wa upinzani kwa madai ya kujikusanya kinyume na kanuni za Covi 19