- Kundi la Wamunyinyi linalenga kutwaa uongozi wa FORD KENYA
- Wetangula ataslia kuwa kinara hadi kundi hilo lifanye mkutano kuidhinisha mageuzi
Seneta wa Bungoma Moses Wetangula sasa anaweza kujipa pumzi baada ya kundi hasimu linalotaka kumuondoa kama kiongozi wa chama cha Ford Kenya kuahirisha mkutano muhimu .
Kundi hilo linaloongozwa na mbunge wa Kanduyi Wafula Wamunyini limeahiriha mkutano wa wajumbe wa kitaifa uliofaa kuandaliwa jumamosi likitaka kuwepo agizo la mahakama .
Hatua hiyo inamaanisha kwamba Wetangula ataendelea kuhudumu kama kinara wa chama hicho hadi wakati wapinzani wake watakapoandaa mkutano wa kuidhinisha maazimio ya kumng’atua .
Mkutano huo pia ulitarajiwa kuidhinisha mageuzi katika uongozi ambayo yalikuwa yametekelezwa mwezi mei .Uchaguzi huo ungekuwa wa kwanza wa Ford Kenya kwa miaka tisa.
Barza kuu la chama hicho liliamua kumtoa Wetangula kutoka nafasi hiyo na kumpa wadhifa huo Wamunyinyi kwa muda kabla ya kuidhinishwa na baraza la wajumbe wa kitaifa . hata hivyo katibu mkuu wa Ford Kenya na mbunge wa Tongaren Eseli Simiyu ambaye yupo katika kambi ya Wamunyinyi amefutilia mbali mkutano huo .