Corona

17 wafariki huku 1,211 wakipatikana na Corona

1,366 NDIO idadi ya walioangamizwa na Corona hadi sasa

Muhtasari

 

 

  • Watu 1,211 wamepatikaa na corona baada ya ampuli 9,304 kupimwa
  • Hata hivyo watu 17 wameaga dunia  na kufikisha 1,366 idadi ya walioangamizwa na Corona .

 

Mutahi Kagwe
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe Mutahi Kagwe

Watu 1,211 wamepatikaa na corona baada ya ampuli 9,304 kupimwa katika saa 24 zilizopita na kufikisha jumla ya  visa vya ugonjwa huo nchini kuwa 76,404 na jumla ya sampuli zilizopimwa zikifika 833,004 .

 Kutoka visa hivyo 1,169 ni wakenya ilhali 42 ni raia wa kigeni .wagonjwa 722 ni wanaume ilhali 489 ni wanawake huku mgonjwa wa umri wa chini akiwa mtoto wa mwezi mmoja na wa umri wa juu akiwa  na miaka 95

 Leo watu 368  wamepona na kufikisha 51,352 idadi ya watu waliopona Corona hadi kufikia sasa 

 

 Hata hivyo watu 17 wameaga dunia  na kufikisha 1,366 idadi ya walioangamizwa na Corona 

 Watu 1,134 wamelazwa katika hospitali mbali mbali nchini huku 6,805 wakiwa chini ya mpango wa kutunzwa nyumbani . wagonjwa 67 wapo katika kitengo cha ICU